KAZI MBALIMBALI ZA IDARA YA UTUMISHI NA UTAWALA
UTANGULIZI:
Idara ya Utawala na Utumishi ni Idara katika taasisi iliyopewa dhamana ya kusimamia Rasilimali Watu pamoja na Rasilimali Mtaji (ikiwa ina maana ya “Asset mbalimbali za halmashauri” katika kutekeleza majukumu hayo Idara inajihusisha na majukumu yafuatayo.
Kusimamia utawala bora
Kuhakikisha watumishi wanatoa huduma bora kwa jamii
Kusimamia uwazi na uwajibikaji
Utii wa sheria
Kusimamia dawati la mteja
Kuratibu vikao na mikutano yote ya kisheria
Kuratibu na kusimamia shughuli zote zinazopatikana katika Mfumo wa “LAWSON”
Kupandisha vyeo watumishi
Kuajiri watumishi wapya
Kubadilisha miundo ya kazi
Kubadilisha hadhi za watumishi
Kuwahamisha watumishi
Kufanya makisio ya bajeti
Kuwaondoa watumishi wanaostaafu kwenye mfumo wa mishahara
Kurekebisha taarifa za watumishi katika mfumo (yanapotokea mabadiliko ama kukosewa).
Kusimamia Kanuni, Sheria na taratibu za Utumishi wa Umma
Kusimamia nidhamu ya watumishi
Kusimamia maadili ya Utumishi wa Umma
Kusimamia na kuratibu utendaj kazi wa watumishi
Kutoa maelekezo na mafunzo juu ya ujazaji wa “OPRAS”
Kusimamia ujazaji wa OPRAS
Kutunza taarifa za watumishi na kuziuisha inapowezekana na kusambaza
Kutunza taarifa kupitia majarada mbalimbali ya watumishi (masijara)
Kusambaza taarifa mbalimbali masijara
Kuwasilisha majibizano “correspondence” mbalimbali kwenye mafaili kutoka Idara moja hadi nyingine (masijara)
Kuandaa Tange za watumishi wote wa Halmashauri “Employees list”
Shughuli zinginezo
Kuhudumia wateja wenye shida tofauti tofauti
Kuidhinisha na kushughulikia mikopo
Kushughulikia madeni ya watumishi
Kushughulikia masuala ya kustaafu
Kusimamia vibarua
Kusimamia usafi
Kuratibu likizo za watumishi
Utunzaji wa vifaa na ofisi
Kuratibu maagizo ngazi za juu
Halmashauri ya Wilaya Simanjiro Bomani street-Orkesumet
Sanduku la Posta: P.o Box 9596,Orkesumet,Simanjiro,Manyara,Tanzania
Simu: Tel:027-29707889
Simu: +255-758350936
Barua pepe: ded@simanjirodc.go.tz
copyright@2016 Halmashauri ya Wilaya Simanjiro.Haki zote zimehifadhiwa