IDARA YA MAENDELEO YA JAMII
Idara ya Maendeleo ya Jamii ni Idara muhimu iliyopo ndani ya Halmashauri ya Itilima. Ndani ya idara hii kuna vitengo mbalimbali vinavyofanya kazi.
Vitengo hivyo ni :-
Kitengo cha Ustawi wa Jamii
Kitengo cha kudhibiti UKIMWI
Kitengo cha Jinsia
Kitengo cha vijana
Kitengo cha kuratibu Asasi Zisizo za Kiserikali
Kitengo cha CHF
KITENGO CHA USTAWI WA JAMII
Kitengo cha Ustawi wa Jamii ni kitengo kinachofanya kazi za kuhudumia jamii kupitia programu mbalimbali za kijamii. Programu zilizopo chini ya Kitengo cha Ustawi wa Jamii ni
Programu za huduma kwa jamii
Kuzishauri idara mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yao ambayo yanailenga jamii mojakwa moja, ikiwemo elimu,afya, kilimo,miundombinu na maendeleo yanayomgusa mwananchi.
Utatuzi wa migogoro na matatizo ya kifamilia
Jamii inayostawi ni ile ambayo inaishi kwa amani na maelewano. Kitengo hiki kipo kwa ajili ya kuunganisha familia . Kitengo hiki hufanya kazi kwa kuzingatia sheria za nchi. Migogoro inayozingatiwa hapa ni :-
Migogoro ya ndoa, ambapo kazi ya Kitengo ni kupatanisha wanandoa kasha warudi kuishi kwa amani
Migogoro kati ya wazazi na watoto wao. Kuna baadhi ya familia ambazo hukosa maelewano kati ya wazazi na watoto wao. Hivyo kitengo hufanya kazi ya kuwapatanisha wazazi hawa na watoto wao.
ANGALIZO:Kitengo hakina mamlaka kisheria kuvunja ndoa za watu,hivyo suluhu inaposhindwa kupatikana, Ofisi hupeleka shauri mahakamani ambapo kwa ajili ya ufumbuzi zaidi.
Programu ya Ulinzi na Usalama wa mtoto
Ulinzi na Usalama wa mtoto ni muhimu sana katika kujenga taifa lililo bora. Programu ya Ulinzi na Usalama wa mtoto katika Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu inatekelezwa ikiwa chini ya Kamati ya Ulinzi na Usalam wa Mtoto. Ulinzi na usalama wa mtoto unafanyika kwa kuzingatia sheria ya mtoto ya mwaka 2009. Ulinzi na usalama wa mtoto ni muhimu ili;-
Kuzuia na kukomesha matendo ya unyanyasaji wa watoto .
Kotokomeza ukiukwaji wa haki za watoto kulingana na sheria ya mtoto ya mwaka 2009.
Kutoa elimu kwa jamii ya ulinzi na usalama wa mtoto
KITENGO CHA KUDHIBITI UKIMWI
Kitengo cha kudhibiti UKIMWI ni kitengo kinachofanya kazi kwa kushirikiana na TACAIDS. Kazi kuu za kitengo hiki ni:-
Kutoa elimu kwa jamii kuhusu UKIMWI na athari zake.
Kutoa elimu juu ya kuepuka maambuzi ya UKIMWI ikiwepo kugawa kondomu pale inapobidi.
Kutoa msaada kwa waathirika wa UKIMWI/VVU kupitia vikundi vyao vilivyosajiliwa kwa kuwapatia ruzuku ili waweze kuendesha shughuli zao za kiuchumi.
Kutoa ushauri kwa waathirika ili wasikate tama ya maisha.
KITENGO CHA JINSIA
Kitengo hiki kipo ili kusaidia wanawake kuweza kujikwamua kiuchumi. Vikundi vya wanawake vilivyosajiliwa huweza kupatiwa mkopo. Ambapo kuna mkopo ambao hutoka moja kwa moja Wizarani kupitia Halmashauri na fedha zinazotengwa na halmashauri katika mapato yake ya ndani ambapo wanawake ambao vikundi vyao vinakidhi vigezo ndio huweza kupewa mikopo.
KITENGO CHA VIJANA
Kuwaunganisha vijana ili waweze kuendesha shughuli zao za kiuchumi kupitia njia ya mikopo. Mikopo hii hitolewa na Halmashauri ,hivyo mara pale fungu linapokuwa tayari vijana ambao vikundi vyao vimesajiliwa huweza kupatiwa mikopo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
KITENGO CHA KURATIBU ASAZI ZISIZO ZA KISERIKALI
Kitengo hiki kinahusika katika kuratibu shughuli za maendeleo zinazofanywa na mashirika yasiyo ya ki-serikali.
KITENGO CHA CHF
Kitengo hiki hufanya kazi kwa kushirikiana na menejiment ktika kusimamia na kuratibu shughuri zote za Mfuko wa Afya ya jamii ikiwemo kuhamashisha wananchi kujiunga,kupata dawa na kupewa tiba kwa jamii ambayo inahusika.
Halmashauri ya Wilaya Simanjiro Bomani street-Orkesumet
Sanduku la Posta: P.o Box 9596,Orkesumet,Simanjiro,Manyara,Tanzania
Simu: Tel:027-29707889
Simu: +255-758350936
Barua pepe: ded@simanjirodc.go.tz
copyright@2016 Halmashauri ya Wilaya Simanjiro.Haki zote zimehifadhiwa