Thursday 5th, December 2019
@Ukumbi wa Halmashauri
Kamati ya lishe wilayani yakaa na kuweka mikakati kadha wa kadha juu ya kupambana na tatizo la utapia mlo kwa watoto na kuhakikisha wananchi wa wilaya ta simanjiro wanapata mlo kamili
Pamoja na kuweka mikakati hiyo Afisa Lishe wilaya Bi Winifrida Chacha alipata fursa ya kusoma kazi zilizofanyika katika kipindi cha robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2018/2019
Aidha kikao hicho cha lishe kimeazimia watendaji wa vijiji kusimamia miradi ya kilimo cha mboga mboga na matunda hasa vinavyoanzishwa na wadau mbalimbali ili viweze kuendelezwa
Kikao hicho pia kilitoa maelekezo kwa idara ya mifugo na uvuvi kutoa elimu ya ufugaji bora wa kuku wa mayai na nyama katika kata ya orkesumet na kwa wajumbe wa kamati ya lishe ili kupata wafugaji bora wa kuku ambao watatumika kutoa elimu katika kata zingine za wilaya ya simanjiro.
Imeandaliwa na kuhaririwa na :
Kitengo cha Teknolojia ya Habari mawasiliano na Uhusiano
Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro
S.L.P 9596,
Orkesumet,Simanjiro
Barua Pepe: ded@simanjirodc.go.tz
Tovuti: www.simanjirodc.go.tz
Halmashauri ya Wilaya Simanjiro Bomani street-Orkesumet
Sanduku la Posta: P.o Box 9596,Orkesumet,Simanjiro,Manyara,Tanzania
Simu: Tel:027-2552225
Simu: +255-758350936
Barua pepe: ded@simanjirodc.go.tz
copyright@2016 Halmashauri ya Wilaya Simanjiro.Haki zote zimehifadhiwa