Idara ya kilimo ina jukumu la kuhamasisha uzingatiaji wa kanuni za kilimo bora, utumiaji sahihi wa pembejeo za kilimo, kutoa elimu ya hifadhi ya chakula pamoja na kuhakikisha wakulima wanaunganishwa na masoko ya mazao yao bila kulanguliwa. Idara hii pia husimamia miradi mbalimbali ya maendeleo inayohusu umwagiliaji, ushirika pamoja na matumizi endelevu ya rasilimali za kilimo na miundombinu yake. Wilaya ya Simanjiro ina jumla ya eneo la kilimo lipatalo ekari 446,000 na eneo linalotumika ni 244,000 kwa mazao ya chakula na biashara. Kati ya ekari zinazolimwa, ekari 26,375 zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji na zinazotumika hadi sasa ni ekari 7,725. Mazao yanayolimwa ni yale ya mboga mboga na nafaka kama mpunga, mahindi na maharage.
Wilaya ina miradi mikubwa ya umwagiliaji inayofadhiliwa na JICA kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania ambayo inagharimu kiasi cha Tsh. 1.8bil. mchanganuo wa miradi hiyo katika skimu za Ngage, Lemkuna na kambi ya Chokaa ni kama inavyooneshwa kwenye jedwali hapa chini.
Jedwali namba 3. Miradi ya Umwagiliaji Ngage, Lemkuna na Kambi ya Chokaa
S/N
|
JINA LA MRADI
|
UTEKELEZAJI
|
FEDHA ILIYOIDHINISHWA
|
FEDHA ILIYOTUMIKA
|
MAONI
|
1
|
Skimu ya umwagiliaji Ngage
|
|
Tshs. 698,000,000/=
|
Tshs. 519,840,000/=
|
Mvua zilizokuwa zikinyesha zimekuwa zikizuia ujenzi wa mradi
|
2
|
Skimu ya umwagiliaji Lemkuna
|
|
Tshs. 569,000,000/=
|
Tshs. 66,338,376/=
|
Kasi ya mkandarasi kutekeleza mradi ni ndogo sana ikilinganishwa na muda uliobaki. Kikao cha Site Meeting kilichofanyika tarehe 11/04/2018 kimemtaka mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi na kuwa hakutakuwa na muda mwingine wa kumuongezea kukamilisha kazi Mei 2018
|
3
|
Skimu ya Umwagiliaji Kambi ya Chokaa
|
|
Tshs. 629,000,000/=
|
Tshs. 86,010,185/=
|
Utekelezaji wa mradi umekuwa na changamoto kubwa ya muelekeo wa mfereji. Wananchi wanalalamika kuwa njia ya sasa haitawanufaisha kwani mfereji unaambaa na mto. Wanataka usanifu ufanyike upya ili muelekeo wa mfereji ubadilishwe ili uweze kumwagilia maeneo yenye mashamba mengi.
|
Katika kipindi cha mwaka 2017/18 baada ya kuona hatua za ufanisi wa mradi wa skimu ya Ngage, wafadhili wa miradi hii yaani JICA wameamua kuongeza kiasi cha fedha kuboresha zaidi skimu hii na tayari zabuni zimeshatangazwa na ofisi ya kamishna wa Tume ya Umwagiliaji kanda ya kati kwenye gazeti la Dailynews la tarehe 12 Aprili 2018.
Halmashauri ya Wilaya Simanjiro Bomani street-Orkesumet
Sanduku la Posta: P.o Box 9596,Orkesumet,Simanjiro,Manyara,Tanzania
Simu: Tel:027-29707889
Simu: +255-758350936
Barua pepe: ded@simanjirodc.go.tz
copyright@2016 Halmashauri ya Wilaya Simanjiro.Haki zote zimehifadhiwa